Kichekesho Karibu katika mtandao wako uupendao unaokupa burudani kwa kukuwezesha kujisomea vichekesho mbalimbali. Usipitwe na vichekesho vikali kila siku!

Vichekesho Huyu dogo ni noma! Soma..!

kichekesho: "MWALIMU NA MWANAFUNZI.\n\nMtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.\n\nMwalimu: Kwa nini unasema hivyo?\n\nMtoto: Nina akili…\n\nBasi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya….\n\nMwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?\n\nDogo: Yatabaki 19.\n\nMwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.\n\nDogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.\n\nMwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.\n\nDogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.\n\nMwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?\n\nDogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.\n\nMwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?\n\nDogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.\n\nMwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?\n\nDogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.\n\nMwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuu….\n😆😆😆😆😆😆😆😆"
jina: ''

Vichekesho Cheki alichokifanya huyu jamaa baada ya kukabwa simu..!

kichekesho: 'Foleni ndeeeeefu jamaa yupo kwenye daladala anaenda kazini kaona heri amuandikie boss wake msg kumtaarifu kuwa atachelewa ile anatakubofya SEND kibaka akaipitia simu. Jamaa kaishia kupga kelele "bonyeza send, bonyeza send wewe" abiria wote hawana mbavu'
jina: ''

Vichekesho Kwa nini watu hawapendi hesabu!! Sababu hii hapa!

kichekesho: "AL-SHABAB\nAL-QAEDA\nKwenye MATHEMATICS pia kuna kundi linaitwa\n\n\"AL-GEBRA\"\n\n😂😂😂😂\n🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻🚶🏻\nKumbe ndo maana wengine hawapendi hesabu coz kuna element za ugaidi"
jina: ''

Vichekesho Cheka kidogo hapa..!

kichekesho: "Kasuku alisimama mlango wa kuingia supermarket wakapita wanawake watatu akasema nyeupe, nyekundu, kijani. Wale wanawake wakatatizika baada ya mda wakajua ni chupi walizovaa. Wakasema basi kesho tubadilisheni. Siku ya pili wakapita tena kasuku akasema nyeusi, manjano, zambarau. Loh! Wanawake wakastaajabu sana. Wakasema lazima wamshinde yule kasuku kwa hekima. Wakaambiana basi kesho tusivae chupi tuone kama ni kweli anaona mpaka ndani. Siku ilipowadia wakapita mbele ya kasuku akasema- kipilipili, kipara, rasta…\n"
jina: ''

Vichekesho AMRI KUMI ZA CHUO

kichekesho: "1.Hicho ndicho chuo chako usiwe na chuo kingine ila hicho.\n2.Usilitaje bure jna la chuo chako mana utawaumiza wengine.\n3.Ikumbuke cku uliyochaguliwa na kuiheshimu.\n4.Waheshimu tcu, bodi ya mkopo na uongoz wa chuo ili upate kuendelea kuwepo chuon.\n5.Usisapu\n6.Usidisko\n7.Usitumie mkopo ovyo.\n8.Usitaman chuo cha mwenzio\n9.Usitamani fakat ya mwenzio\n10. Usitaman bumu lake wala chochote alichonacho. hahaha chezea chuo weye!"
jina: ''

Vichekesho Mambo ya Mabinti haya

kichekesho: "Binti: Hallow mpenzi, Mambo\n\nJamaa: Poa baby\n\nBinti:Uko wapi?\n\nJamaa: Niko town napata lunch\n\nBinti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi\n\nJamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?\n\nBinti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.\n\nJamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.\n\nBinti: Kwanini dear?\n\nJamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli"
jina: ''

Vichekesho Hawa machizi wamezidi sasa

kichekesho: "Machizi wamekaa sehemu mara ghafla ikapita ndege angani.\nChizi wa kwanza akasema:ndege ile itakua imembeba raisi.\nChizi mwenzie akajibu:hapana imebeba wazungu kama ingembeba raisi tungeona pikipiki zimetangulia mbele…\nda!balaaa"
jina: ''

Vichekesho Maana ya msemo siri haina wawili hii hapa

kichekesho: "📦SIRI HAINA WAWILI📦\n\n👂Imesimuliwa kuwa\n\n🙇Palitokea mtu maskini jina lake ban hashim na alikuwa na mke maisha yake alijishuhulisha katika kilimo.\n\n🌼Siku moja wakati akilima aliokota fungu la dhahabu shambani alilibeba akafurahi na kushukuru licha ya kuwa alikuwa na hofu sana\n\n🌼Kwani alifikiri angelihadithia watu wasingemuamini kwa umaskini wake wangedhani huenda ameiba na hakuna ambae angeweza kuinunua dhahabu hio ila wangemtapeli tu\n\n🌼Aliondoka akiwa ameibeba dhahabu yake katika mfuko akaingia nayo nyumbani kwake na kuificha bila mkewe kujua chochote\n\n🌼Alipofikiria kumwambia mkewe juu ya mali alioipata aliogopea kuwa huenda mkewe akawatangazia majirani kisha wakaibiwa na wezi\n\n🌼Akafikiria sana mwisho akapata ufumbuzi aliingia chooni akakaa muda kisha akamfata mkewake huku akiwa na uwoga\n\n🌼Kisha akamwambia mke wangu ntayokuambia tafadhali iwe siri wala yoyote asijue nae mkewe alimuahidi kuwa angeiitunza siri hio pasi na mtu kujua\n\nAkamwambia nilipoingiaa chooni kujisaidia ghafla walitoka ndege wawili kisha wakakimbia kimaajabu mkewe kuskia hivo alistaajabu😳 kwa lililomtokea mumewe\n\n🌼Siku ya pili mkewe alikwenda kwa jirani yake wa karibu kisha katika stori mara akamwambia shoga angu lililompata mume wangu nila ajabu jana kaingia chooni baada ya kujisaidia wakatoka ndege watatu kisha wakaruka kimaajabu jirani alishangaa kisha akamwambia usiseme mume wangu alinikataza nisihadithie\n\n🌙Ikapita muda jirani nae siku ameketi na watu akawasimulia jamani mnahabari mke wa ban hashim amenisimulia kuwa mumewe aliingia kujisaidia mara wakatoka ndege wanne wakarukaa kimaajabu habari zikazidi kuenea katika mji wao na kila alie hadithia aliongeza ndege mmoja ,3,4,5,6 mpaka ikafika kwa mfalme kuwa kuna mtu kajisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabu\n\n🌼Jambo hili lilimshangaza sana mfalme 👳😳akatuma watu wakamkamate huyu mtu na wamlete kwake ili amuone huenda mtu wa ajabu sana\n\n🌼Walitoka watu 🚶🏃wakamfata wakamwambia mfalme anakuita akashuhudie kwako juu ya habari kuwa wewe umejisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabu\n\n🚶👬Basi Alitoka akaongozana na hao watu huku akiwa amebeba mfuko wake wa dhahabu bila ya watu kujua alichobeba mpaka wakafika mbele ya mfalme\n\n🌼Mfalme 👳akamwambia je ni kweli wewe ndie ulie jisaidia ndege 100 kisha wakaruka kimaajabu?\n\n🌼Ban hashim alicheka😬😆 kisha akamwambia mfalme hizi habari nilimsimulia mke wangu👂 kuwa nilijisaidia ndege wawili nashangaa zimeenea na kila alieambiwa alipomhadithia mwenzake aliongeza ndege mmoja mpaka imefika kwako niliambiwa kuwa nimejisaidia ndege 99 kisha na wewe ukaongeza mmoja wakatimia 100\n\n👳Mfalme kusikia hivo alicheka 👳😆kusikia kisa hichi kisha ban hashim akamwambia mfalme mimi niliokota dhahabu shambani nikaona hakuna ataeweza kuinunua sana watanidhulumu💴💵 au kuniua 🔫na kwako sikuweza kukuletea kwani hawaingii ovyoo watu kwa mfalme ndio nikafanya hivi ili niweze kuja kwako kwa urahisi na dhahabu ni hii akaiweka mbele ya mfalme kisha mfalme alimpa pesa nzuri💰 zilizokuwa sawaa na mali yake akarudi na kuishi kwa furaha na mke wake.\n\n📦Kisa hichi kinafunza kuwa ukiletewa habari✉ na mtu basi ichunguze na usizidishe kitu kwani watu huongeza yao au kupunguza kwa kila wanalolisikia na inatufunza mke kuwa na siri na mumewe na sio kuzitangaza kwa majirani\nKwani habari zinaruka kama mfano wa vumbi kuenea kwa haraka.\n\n🌼Licha ya kuwa ban hashim alipata urahisi wa kuuza dhahabu yake lakini na kama ingekuwa madhara basi angeangamia kwa mdomo wa mkewake🙉🙊.\n\n🚧Mwisho kisa hiki hakikutaja majina ya wahusika kilipo mfikia ban hashim alikisaidia kukitia majina ya wahusika ili kisipoteze sifa yake ya uweneaji😊\n\n🌴🐪KISIWA CHA IMANI🐪🌴"
jina: ''

Furahia vichekesho hivi Vingine sasa!!

Site map

| Classic Funny Posts | Picha kali ya Siku | Vichekesho bomba vya leo | Wazo la Leo | Ackyshine |