# Ulishawahi kupenda kwa namna hii??!!

kichekesho: "Ushawai kumpenda dem na kumfia mazima kiasi kwmb anakwambia ye ana msela lkn we huelewi..unamkazia!!\nInabidi dem asisitize,\"I HAVE ONLY ONE HEART,PLZ, I CANT LOVE TWO MEN\"\nNawewe unaona haiwezekan,unamwambia 'NIPENDE ATA NA KIDNEY'😃😃😙😃😃😃😗😃"
jina: ''

# Huyu dingi na maza ni noma, soma

kichekesho: "DOGO: Mama Jana Baba Alikuja Na Mwanamke Na\nAkaanza Kumtoa Nguo Huku Akimuita Beib…\nBABA: Kwa Hasira Ebu Wacha Kuongea Na Chakula Mdomoni Wewe Mpumbavu Sana Khaa!!!\nMAMA: Eti Nini Hebu Endelea Mwanangu Alafu\nWakafanya Nini Hawa Nguruwe… DOGO: Wakanza Kufanya Kama Vile Mlifanya Na Anko nassoro Wakati Baba Alikua Safari Za\nkikazi…\nMAMA: Kwa Hasira Babako Amesema Uwache\nKuongea Na Chakula Mdomoni We Kweli\nMpumbavu sana…\n"
jina: ''

# Ungekua wewe ungemjibu nini huyu?

kichekesho: "Dogo mmoja baada ya kurudi shule akawa anaongea na baba yake\n\nKa ww\n\nDOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.\nBABA: Kwanini unasema hivyo?\nDOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.\n\nungekua wewe ungemjibu nini"
jina: ''

# Soma hii! SIFA 10 ZA MWANAUME AMBAYE KILA BINTI ANAETAKA KUOLEWA ANGEPENDA AOLEWE NAE

kichekesho: "1. Awe na pesa nyingi\n\n2.Siyo lazima awe mzuri wa sura\n\n3. Ajenge ukweni\n\n4.Awe mpole\n\n5.Asimuonee wivu mke wake\n\n6.Awe mwenye upendo wa dhati\n\n7.Asishike simu ya mke wake.\n\n8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani\n\n9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.\n\n10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake\n\nUKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.\n😂😂😂😂😂😂😂😂"
jina: ''

# Cheki huyu demu alivyoumbuka

kichekesho: 'Demu mmoja aliingia duka la vito vya thamani, akaona pete moja ya dhahabu nzuri sana amabayo ilikuwa kwenye shelf ya chini, wakati anainama apate kuitazama vizuri kwa bahati mbaya (au nzuri!), shuzi likamtoka- druuuuuu, soni ikamuingia huku akigeuka haraka kuangalia kama kuna yeyote dukani pale ameliskia shuzi lake, macho yakagongana na mwenye duka ambaye alikuwa karibu huku uso ukiwa umejaa tabasamu zito, mwana mama hakuwa na uhakika kama amesikika au hakusikika, akaona atumie nafasi ile kuyeyusha…Akauliza "Hii pete bei gani?" . Jamaa mwenye duka, huku akiangua kicheko, akajibu "Umeiona tu umejamba, je nikikuambia bei yake si utakunya kabisa?"'
jina: ''

# Mwalimu mkuu katoa kali ya mwaka

kichekesho: "Mwalimu kauliza swali darasani\nwanafunzi wataje\nkazi za wazazi wao:\nTINA: mimi baba yangu\nmfanyabiashara mama\nyangu mwalimu.\nMWALIMU: Safi, haya juma\nJUMA: Baba yangu dereva mama\nyangu hafanyi\nkazi.\nMWALIMU: Vizuri, haya Zogo.\nZOGO: Mimi mama yangu malaya\nanajiuza baba\nsimjui.\nMWALIMU: Pumbavu wewe, nenda\nofisini kwa\nmwalimu mkuu ukamueleze upuuzi\nwote\nuliosema hapa. Zogo anaenda ofisini\nanarudi\nhuku anatabasamu na anakula\nbiskuti.\nMWALIMU: Mwalimu mkuu kakupa\nadhabu gani?\nZOGO: Kaniambia nimpe namba ya\nmama…\n\n😂\n"
jina: ''

# Wazo la leo!

kichekesho: "📢WAZO LA JIONI HII 📢\n\nKAMA MWAKA JANA ULIPIGA HATUA NA HUJAFIKIA MALENGO MWAKA HUU PIGA MSAMBA😝"
jina: ''

# Mvua zazua kasheshe! Soma hii..

kichekesho: "MVUA ZAZUA KASHESHE.. SIKILIZA HII..\nBaba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani\nMAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ?\nBABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia\nMAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia\nBABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan\nMAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.\nBABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15\nBaada ya dk 15 Baba kafika nyumban.\nMAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro?\nBABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..\n\nKama umeipenda shea na rfiki zakooo….."
jina: ''

# Wasichana wa leo ni kazi kwelikweli

kichekesho: "Jamaa yupo ndani ya Range rover yake mpya na msichana ambaye ni mpenzi wake.\n\n#Jamaa: kuna siri flani nimeitunza moyoni mwangu kwa muda mrefu na nikaona kama nitakuambia lazima utaniacha.\n\n#Msichana: siri gani hiyo mpenzi wangu?\n\n#Jamaaa: nimeoa.\n#Msichanaa: Hɛɛɛɛɛɛɛɛ! We umenishtua sana,mm nilifikiri hili gari sio lako!\n🙆🙆🤗🤗"
jina: ''

# Soma hii! Je huyu kapona?

kichekesho: 'Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?'
jina: ''

# Maana ya msemo siri haina wawili hii hapa

kichekesho: "📦SIRI HAINA WAWILI📦\n\n👂Imesimuliwa kuwa\n\n🙇Palitokea mtu maskini jina lake ban hashim na alikuwa na mke maisha yake alijishuhulisha katika kilimo.\n\n🌼Siku moja wakati akilima aliokota fungu la dhahabu shambani alilibeba akafurahi na kushukuru licha ya kuwa alikuwa na hofu sana\n\n🌼Kwani alifikiri angelihadithia watu wasingemuamini kwa umaskini wake wangedhani huenda ameiba na hakuna ambae angeweza kuinunua dhahabu hio ila wangemtapeli tu\n\n🌼Aliondoka akiwa ameibeba dhahabu yake katika mfuko akaingia nayo nyumbani kwake na kuificha bila mkewe kujua chochote\n\n🌼Alipofikiria kumwambia mkewe juu ya mali alioipata aliogopea kuwa huenda mkewe akawatangazia majirani kisha wakaibiwa na wezi\n\n🌼Akafikiria sana mwisho akapata ufumbuzi aliingia chooni akakaa muda kisha akamfata mkewake huku akiwa na uwoga\n\n🌼Kisha akamwambia mke wangu ntayokuambia tafadhali iwe siri wala yoyote asijue nae mkewe alimuahidi kuwa angeiitunza siri hio pasi na mtu kujua\n\nAkamwambia nilipoingiaa chooni kujisaidia ghafla walitoka ndege wawili kisha wakakimbia kimaajabu mkewe kuskia hivo alistaajabu😳 kwa lililomtokea mumewe\n\n🌼Siku ya pili mkewe alikwenda kwa jirani yake wa karibu kisha katika stori mara akamwambia shoga angu lililompata mume wangu nila ajabu jana kaingia chooni baada ya kujisaidia wakatoka ndege watatu kisha wakaruka kimaajabu jirani alishangaa kisha akamwambia usiseme mume wangu alinikataza nisihadithie\n\n🌙Ikapita muda jirani nae siku ameketi na watu akawasimulia jamani mnahabari mke wa ban hashim amenisimulia kuwa mumewe aliingia kujisaidia mara wakatoka ndege wanne wakarukaa kimaajabu habari zikazidi kuenea katika mji wao na kila alie hadithia aliongeza ndege mmoja ,3,4,5,6 mpaka ikafika kwa mfalme kuwa kuna mtu kajisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabu\n\n🌼Jambo hili lilimshangaza sana mfalme 👳😳akatuma watu wakamkamate huyu mtu na wamlete kwake ili amuone huenda mtu wa ajabu sana\n\n🌼Walitoka watu 🚶🏃wakamfata wakamwambia mfalme anakuita akashuhudie kwako juu ya habari kuwa wewe umejisaidia ndege 99 kisha wakaruka kimaajabu\n\n🚶👬Basi Alitoka akaongozana na hao watu huku akiwa amebeba mfuko wake wa dhahabu bila ya watu kujua alichobeba mpaka wakafika mbele ya mfalme\n\n🌼Mfalme 👳akamwambia je ni kweli wewe ndie ulie jisaidia ndege 100 kisha wakaruka kimaajabu?\n\n🌼Ban hashim alicheka😬😆 kisha akamwambia mfalme hizi habari nilimsimulia mke wangu👂 kuwa nilijisaidia ndege wawili nashangaa zimeenea na kila alieambiwa alipomhadithia mwenzake aliongeza ndege mmoja mpaka imefika kwako niliambiwa kuwa nimejisaidia ndege 99 kisha na wewe ukaongeza mmoja wakatimia 100\n\n👳Mfalme kusikia hivo alicheka 👳😆kusikia kisa hichi kisha ban hashim akamwambia mfalme mimi niliokota dhahabu shambani nikaona hakuna ataeweza kuinunua sana watanidhulumu💴💵 au kuniua 🔫na kwako sikuweza kukuletea kwani hawaingii ovyoo watu kwa mfalme ndio nikafanya hivi ili niweze kuja kwako kwa urahisi na dhahabu ni hii akaiweka mbele ya mfalme kisha mfalme alimpa pesa nzuri💰 zilizokuwa sawaa na mali yake akarudi na kuishi kwa furaha na mke wake.\n\n📦Kisa hichi kinafunza kuwa ukiletewa habari✉ na mtu basi ichunguze na usizidishe kitu kwani watu huongeza yao au kupunguza kwa kila wanalolisikia na inatufunza mke kuwa na siri na mumewe na sio kuzitangaza kwa majirani\nKwani habari zinaruka kama mfano wa vumbi kuenea kwa haraka.\n\n🌼Licha ya kuwa ban hashim alipata urahisi wa kuuza dhahabu yake lakini na kama ingekuwa madhara basi angeangamia kwa mdomo wa mkewake🙉🙊.\n\n🚧Mwisho kisa hiki hakikutaja majina ya wahusika kilipo mfikia ban hashim alikisaidia kukitia majina ya wahusika ili kisipoteze sifa yake ya uweneaji😊\n\n🌴🐪KISIWA CHA IMANI🐪🌴"
jina: ''

# Soma! Kati ya demu na mshikaji, nani anajeuri?

kichekesho: "\"MAENEO FLANI ya KISHUA\"\n\n-Mshikaji kamwona demu mkali\nanakatiza kitaa akamkubali akaamua\namfuate amtemee cheche\n\nMSHIKAJI- mambo dada?\n\nDEMU- pouwa\n\nMSHIKAJI-\numependezaa!!!\n\nDEMU- asante.\n\nMSHIKAJI- unaweza ukanisaidia\nnamba\nyako ya simu……..\nmaana duh\nnmekukubali\nkinyama.\n\nDemu baada ya kuambiwa vile\nakazama kwenye pochi lake akatoa\nnoti ya\nsh.10000 akaandika namba yake\nkwenye\nnoti akampa mshikaji.\n\nMshikaji kapokea ile noti kachana\nsehem\niliyoandikwa namba halafu\nkamrudishia\nDemu noti yake..!!!\n\nNANI ANA DHARAU\nNA NANI JEURI..\nDEMU AU MSHIKAJI??!\n\nJipatie.JPG"
jina: ''

# Maana ya mchepuko usiyoijua

kichekesho: "Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.\nNyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.\n\nMara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.\n\nTv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.\n\nTv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.\n\nGharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.\n\nTv ina remote lakini Simu haina.\n\nKitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.\n\nUnaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.\n\nYa mwisho na ya kuzingatia\n\nTv haina Virusi lakini Simu inayo."
jina: ''

# Angalia watoto wanavyopenda pilau! Utoto raha kwelikweli....!

kichekesho: "Leo nimepulizia Air Fresh yenye Harufu ya Pilau nyumbani kwangu sasa watoto wa Jirani wamehamia Mlangoni kwangu ndio wanacheza hapo. Kila nikitoka wananisalimia. Mama yao ndio kanimaliza kabisa nimetoka akaniambia\n\"Kumbe wewe ni Mpishi mzuri, Hongera\"\n\nImebidi nisirudi nyumbani maana wale watoto wanaweza kuingia ndani kabisa na pilau hakuna.\n\n#UTOTO RAHA 😂\n\n😂😂😂😂👆🏻👆🏻👆🏻"
jina: ''

# Cheki alichokifanya huyu jamaa baada ya kukabwa simu..!

kichekesho: 'Foleni ndeeeeefu jamaa yupo kwenye daladala anaenda kazini kaona heri amuandikie boss wake msg kumtaarifu kuwa atachelewa ile anatakubofya SEND kibaka akaipitia simu. Jamaa kaishia kupga kelele "bonyeza send, bonyeza send wewe" abiria wote hawana mbavu'
jina: ''

# Mambo ya Mabinti haya

kichekesho: "Binti: Hallow mpenzi, Mambo\n\nJamaa: Poa baby\n\nBinti:Uko wapi?\n\nJamaa: Niko town napata lunch\n\nBinti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi\n\nJamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?\n\nBinti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.\n\nJamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.\n\nBinti: Kwanini dear?\n\nJamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli"
jina: ''

# Kauli 10 MBAYA za walimu darasani, unakumbuka ipi kati ya hizi??

kichekesho: "1:Mkimaliza kuongea niambieni niendelee kufundisha\n\n2:Baba yako kauza ng'ombe ili alete ng'ombe mwingine shule\n\n3:Kama unajua kuliko mimi njoo ufundishe wewe\n\n4:Ulikuja peke yako na utaondoka peke yako\n\n5:Hata msiponisikiliza mshahara wangu uko pale pale\n\n6:Baba yako anahangaika kulipa ada wewe unafanya utumbo tu\n\n7:Hata nikeshe nafundisha wengine ni mizigo hawatoki na lolote\n\n8:Tunavisaidia tu kwan vikifanikiwa mbelen hata salam vinatoa?\n\n9:Bichwa kubwa ubongo nukta\n\n10:Wengine hapa wamekuja kukua tu"
jina: ''

# Dada azimia kanisani akifunga ndoa

kichekesho: "NDOA inafungwa KANISANI Mchungaji akauliza-\nYeyote mwenye Pingamizi La Ndoa hii kufungwa aje Mbele, KIBABU kikasimama na kwenda Mbele,\nBi harusi akaanguka na akazimia ghafla!😭😭😭\nMchungaji- Tuambie Babu Pingamizi Lako!\nBabu-Nimeamua kuja mbele,kule nyuma sisikii vizuri! watu hoiiii!!\n\nhata mimi hoi…😃😃😃😃😃😃😃"
jina: ''

# HABARI MPASUKO.. Nyoka wa ajabu agundulika

kichekesho: "jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea… huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..\n\nnyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..\n\nasanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hii…"
jina: ''

# Angalia ilivyokua Mhindi kwenye mtihani wa kiswahili anaambiwa amalizie methali

kichekesho: "Mhindi kwenye mtihani wa kiswahili anaambiwa amalizie methali:\n(a)Nyani haoni…..valisa miwani!\n(B)Debe tupu….weka dengu!\n(c)Masikini akipata….iko acha iba!\n(d)Penye kuku wengi…chinja bili,tatu!\n(e)Asiyesikia la mkuuu….peleka yeye polisi!\n(f)Penye wengi……iko kutano ya chadema!"
jina: ''

# Kisa cha mvuvi maskini na mkewe malaya

kichekesho: "Mvuvi mmoja alikua akiishi na mke wake huku\nakiwa hajui kama mkewe malaya,\nLeo hii kamuaga mkewe baada ya kuondka\nmkewe akaanza kuingiza wanaume kama\nkawaida\nHawara 1;nakupenda\nMke Wa Mvuvi;oke, Nipe Penz Haraka Kabla\nMume wngu hajarudi.\nHawara 1;oke!\nBasi picha likaanza wakati wanaendelea mara\nmlango ukagongwa, akamwambia hawara mume\nwangu huyo jifiche darini jamaa akafanya„ mke\nwa mvuvi akaelekea mlangon kumbe alikua\nhawara 2.\nmke wa mvuvi; aaahaa kumbe ni wewe nilijua\nmume wangu bas njo haraka kabla mume wangu\nhajarudi..\npicha likaendelea huku wa darini akiona vyote,\nmlangon kukagongwa\nmke wa mvuvi; mume wangu hyo jifiche uvungun\njamaa akafanya kisha mke akajikoki kumpokea\nmumewe,\nmke wa mvvi; oooh! mume wngu pole umechoka\neeh leo umepata samaki mkubwa nashukuru sana\ntulikua hatuna mboga\nmvuvi;usinishukuru mimi mshukuru aliye juu.\nhawara 1; sipo mwenyewe mwingine yupo\nuvunguni…"
jina: ”

# Unakumbuka enzi za utoto

kichekesho: "SHERIA ZETU ZA MPIRA ZA UTOTONI:\n1.Mwenye mpira Lazima acheze ata kama hajui mpira\n2.Dogo mnene Lazima awe golikipa\n3.Mwenye mpira ataamua nan acheze na nan asicheze\n4.kama haujashiriki kufuma mpira unaweza ucpate namba\n5.Ukichaguliwa mwishon ujue uwezo wako ni mdogo kuliko wote\n6.Mwenye mpira akikaclika mpira umeisha\n7.Inaruhusiwa kubadili golikipa kama ikitokea penat na baada ya apo ataendelea kudaka yule yule\n8.Mechi itaisha pale giza linapoingia\n9.wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka\n10.yule mtaalam wa soka {KM MIMI } huwa hakoc namba ata cku moja!\nUkiikumbuka lazima utabasam!"
jina: ''

# Duh! angalia huyu baba na msichana wake

kichekesho: "Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia hivi:-\n\nMSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa \"DADDY IS AT HOME?\" by Ngozi Okafor\n\nMVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha maombi kama kinaitwa \"WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?\" by Ngũgĩ wa Thiong'o\n\nMSICHANA: Aaah! Hicho sina ila ninacho kimoja kinaitwa \"UNDER THE MANGO TREE\" by Chimamanda Adichie\n\nMVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p'Bitek kile kinachoitwa \"CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE\" Utakapokuja shule.\n\nMSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa \"I WON'T LET YOU DOWN\" by Chinua Achebe\n\nBaba mtu akawatazama kisha akasema\n\nBABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli\n\nMSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana yupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!\n\nBABA: Sawa! Usisahau kumpatia na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa \"I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU'VE BEEN SAYING\" by Shakespeare!\n\nNa kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa \"IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED\" by Wole Soyinka."
jina: ''

# Bangi ni noma! soma hii..!

kichekesho: "kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi…kiberiti kikawaishia…wakamtuma mwenzao akatafute kingine…bangi lilikuwa limemkolea…akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…\n\nMSHIKAJI:oyaaa wanangu eeeh…niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe…..\n\nWENZAKE:baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti"
jina: ''

# Angalia kilichompata huyu katika ziara za kushtukiza

kichekesho: "Mimi Nimecheka sana\n👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇\n\nZIARA ZA KUSHTUKIZA😀😀\nMimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.\n\nNikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza. Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, “Mzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapi” Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu. Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, “Mume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyo”. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa. Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, “Salama kaka unasemaje?” Jibu likanitoka “Samahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yangu” Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani"
jina: ''

# Status za Whatsapp za wabongo na wazungu

kichekesho: "STATUS ZA WAZUNGU kwenye Whatsapp vere vere kliaaa…\n👉sick\n👉at movie 👉 in a meeting2\n👉 kind of happy„ 👉busy\n👉available\n👉Driving\n👉sleeping\n\nSTATUS ZA WABONGO SASA MBUTA NANGA MBONGO NGAFU\n\n\"Akutake nani una shepu la Kitorondo utaishia kumegwa na kuachwa\n\n\"Watu tuna nyota za Chips Mayai sio wewe mwenye Nyota ya Punda,halulaaa\"\n\n👌Kantangazeee ndo Kwanza naanza na ntakukomesha Mwanaharamu we!\n\n😍 I love yu so much ur my only one,No one lyk yu and I mean it 🎶 Yu ma numba1 ma sweet sweet namba1 roho yangu mama\n\n👍 Asante 😍 vimenitoshaaa tena kama ulijua 😘😘😘😘😘,\n\n💪 unajifanya simba kumbe nyau mimi ndo maji kama hujanioga utaninywaa,\n\n🙈 nauza Ubuyu kwa bei nafuuu kama unataka inbox me plz\n\n😔 poleee jaman utapona wangu,,,\n\n💪 utalijua jiji na chuki zako walingia na tako wakati hadi nyani analo kitu sura dada…\n\n😡 usinisemeshe usiniongeleshe tena utaniambia vizur ulikuwa wapi..\n\n😷 mdomo kaumbiwa mwanadamu ongeeni nyie me sijali ya wanafiki nafanya yangu huna hadhi ya kujibiwa na mimi\npamoja na ya kwako uloweka🙈😆😆😆"
jina: ”

# Mambo ya PLASTIC SURGERY ni shida! Ona kilichompata huyu

kichekesho: "Jamaa alionekana Mnyooooonge sana ikabidi mpita njia amuulize…\n\nKaka, mbona u mnyonge hivyo?\"\nJamaa : 'aaaaah we niache tu, kuna rafiki yangu nimemkopesha laki tano akafanye PLASTIC SURGERY ya uso, Mwanaharamu sasa nashindwa kumtambua!!!\n😂😂😂😂😂😂"
jina: ''

# Hawa machizi wamezidi sasa

kichekesho: "Machizi wamekaa sehemu mara ghafla ikapita ndege angani.\nChizi wa kwanza akasema:ndege ile itakua imembeba raisi.\nChizi mwenzie akajibu:hapana imebeba wazungu kama ingembeba raisi tungeona pikipiki zimetangulia mbele…\nda!balaaa"
jina: ''

# Cheki alichosema huyu baba kwa mwanae baada ya mwanae kumwambia anataka kujiua

kichekesho: "Mtoto:Baba nitumie pesa ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya sana la sivyo najinyonga.\nBaba: Huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga utapunguza Bajeti, kopa Kamba dukani kwa Mangi nitalipa nikija kuchukua Maiti yako, Mungu akulaze mahali pema peponi Mwanangu….."
jina: ''

# Cheki huyu mke alivyofanya ujinga kwa wivu wake..!

kichekesho: "Mke: Hivi mume wangu una wanawake wangapi huko nje?\nMume: Kama nywele za kichwa changu.\nMke akachukua nguo zake akaondoka, Kufika njiani akakumbuka mumewe alikuwa na kipara Akaanza kurudi kwa mumewe."
jina: ''

# Ona kilichotokea baada ya baba mmoja kumpaka sumu mke wake kwenye matiti

kichekesho: "Baba mmoja Juzi alimpaka Sumu Mke wake kwenye Matiti akiwa amelala ili Mtoto akinyonya afe kwani alihisi sio wa kwake, akaondoka kwenda kazini aliporudi akakuta house boy amekufa,\nusiniulize alikufaje. Mie mambo ya umbea sipendi niliondoka zangu mapemaaa!!😅😅😅😅\n\n😝😝😝😝😝😝"
jina: ''

# Je, wajua! maajabu ya kuku na n'gombe wa Whatsapp

kichekesho: "JE WAJUA?\n\nJe wajua kwamba kuku wa kwenye Whatsapp anamzidi tembo ukubwa? 🐓👉🏽🐘.\n\n😂😂😂Maajabu!"
jina: ''

# Angalia huyu bibi alivyomfanyia huyu jamaa

kichekesho: "Bibi na Babu walisafiri wakielekea kwa mtoto wao ambae hawajamuona zamani.\n\nWalipofika njiani wakawa wamechoka Sanaa. Wakaamua kutafuta hotel ili walale.\n\nWakakubaliana walale kwa masaa 4. Wakalala, Walipoamka, mfanyakazi wa Hotel akawatoza Tsh. 500,000/=\n\nWale wazee wakashangaa hata kama ni hotel ya kisasa lakini sio laki tano kwa masaa 4.\n\nBabu akagoma kulipa akasema aitiwe meneja.\n\nMeneja akaja kuwasikiliza\n\nBabu: \" Kwanini bili ni kubwa hata kama ni hotel ya kisasa?\"\n\nManager;\"kuna maswiming puli, ya kisasa \"\n\nBabu; \"Lakini hatukuyatumia\"\n\nManager; \"Ah ah ah. Lakini mungeweza kama mngetaka\"\n\nBabu: \"Hata hivo bado haithamini kuwa laki 5\"\n\nmeneja: \"Pia Kuna waimbaji kutoka sauzi, Uganda , Congo\"\n\nBabu: \"Lakini sisi hatukuwasikiliza\"\n\nMeneja: \"Ndiooo. Lakini mngeweza kama mngetaka\"\n\nBabu; aka give up na kumwambia mkewe andika cheki uwape„\n\nBibi akaandika akampa meneja.\n\nMeneja anaangalia anaona sh. 50,000\n\nAkashangaa na kusema. \"VP mbona hamsini'\"\n\nBibi akajibu \"450,000 ya kulala na mimi\"\n\nMeneja akajibu; \"Lakini sijalala\"\n\nBibi :\"ungeweza kama ungetaka\""
jina: ”

# AMRI KUMI ZA CHUO

kichekesho: "1.Hicho ndicho chuo chako usiwe na chuo kingine ila hicho.\n2.Usilitaje bure jna la chuo chako mana utawaumiza wengine.\n3.Ikumbuke cku uliyochaguliwa na kuiheshimu.\n4.Waheshimu tcu, bodi ya mkopo na uongoz wa chuo ili upate kuendelea kuwepo chuon.\n5.Usisapu\n6.Usidisko\n7.Usitumie mkopo ovyo.\n8.Usitaman chuo cha mwenzio\n9.Usitamani fakat ya mwenzio\n10. Usitaman bumu lake wala chochote alichonacho. hahaha chezea chuo weye!"
jina: ''

# Mbongo kwa sifa! cheki kilichompata

kichekesho: "\nMbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.\n\nWakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.\n\nBasi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.\n\nWakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.\n\nWakaingia msituni kila mtu njia yake.\n\n… Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.\n\nMkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala nini… alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.\n\nWakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, “Vipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?”\n\nMkenya akamjibu: “Mkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!”"
jina: ''

# Angalia mapenzi ya siku hizi! ni shida..!

kichekesho: "Jamaa: I love you sweetie\nBinti: I love you too, ila ha2tafanya mapenz had utaponioa\nJamaa: Hilo halina shida, ila usiniombe hela hadi siku ntapokuoa\nBinti: Heeeeeee! baby hutaniwi?!"
jina: ''

# Hapa sasa shida ni ya nani? soma hii

kichekesho: "Umeshawahi saidiwa homework na mzazi halafu unapata zero?\n\nHapo ndio unajua shida siyo wewe\n\n😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😂😂"
jina: ''

# Alichosema mchungaji baada ya kufungisha ndoa mashoga wawili

kichekesho: 'Mchungaji mmoja baada ya kuwafungisha ndoa "MASHOGA" wawili alipata wakati mgumu kutamka kuwa "sasa ninyi ni MKE na MUME" atafanyaje wakati wote ni wanaume? mchungaji akapiga moyo konde na kusema "tangu sasa ninyi ni MAN UNITED"'
jina: ''

# Angalia mvulana fala kuliko wote

kichekesho: "ALITOKEA MVULANA MMOJA:\n😂😂😂😂\n\nMVULANA: Daktari, rafiki yangu wa kike ni mjamzito, lakini mara zote nimekua nikitumia kinga. Inawezekanaje hii?\n\nDAKTARI: Ngoja nikusimulie hadithi. Kulikua na Muindaji ambaye alikua anabeba bunduki kila aendako. Siku moja, alichukua mwamvuli badala ya bunduki na akaenda nayo. Ghafla akatokea Simba mbele yake. Ili amtishie Simba, muindaji akatumia mwamvuli na kummiminia risasi Simba. Simba akafa palepale!\n\nMVULANA: Sio kweli!! Lazima kulikua na mtu mwengine pembeni aliyempiga risasi Simba.\n\nDAKTARI: Nashukuru umeelewa somo!!😂\n\n😂😂😂😂😂😂😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃"
jina: ''

# Misemo mikali ya leo

kichekesho: "\n1. Ati wee ni m-black mpaka ukiingia kwa dinga(gari), dirisha zinakuwa tinted!\n\n2. Kwenu kuchafu mpaka mende zinatema mate.\n\n3. Vile wewe mfupi, ukipiga picha ya passport inatokea full.\n\n4. Ati(house) yenu ina gate lakini hakuna fence.\n\n5. Baba alienda ku buy ngombe akaona ikikojoa akasema sitaki hiyo imetoboka.\n\n6.Wee mblack mpaka ukikutana na mzungu afternoon anakusalimia: Good evening.\n\n7. Mko wengi kwa house mpaka kuna rush hours na kukinyesha kunakuwa na jam.\n\n8. Paka yenu noma mpaka ikishika panya inaomba chumvi, fork na pilipili.\n\n9. We ni mrefu mpaka ukikunywa maziwa inafika kwa tumbo ikiwa mgando.\n\n10.Wewe ni mweusi ukikanyanga makaa unawacha footprint nyeusi.\n\n11. Kwenyu mkikunywa maji mnaitisha toothpick\n\n12. We ni mbishi hadi ulikataa kuzaliwa uchi\n\n13. Kwenu kuna insecurity ikifika usiku hadi geti mnaingiza ndani\n\n14. Kwenu ni wengi sana hadi mmeweka round about ndani.\n\n15. Wewe ni mlafi hadi maji uliyochemshia mayai unayafanya supu.\n\n16. We ni mjinga sana hadi blood test ulifeli.\n\n17. Una chogo refu hadi ukigeuka haraka unaweza kuliona.\n\n18. Una kichwa kikubwa hadi ukiingia kwenye daladala konda anakwambia \"abiria usiingie na mizigo, tunaweka juu kwenye carrier"
jina: ''

page 1 of 3123next »